Tuesday, August 6, 2013



HISTORIA YA MAISHA YANGU
Mimi naitwa Abeid     Yusuph   Mehuluso Lukanga.
Kabila-makonde
Dini-islamic
Elimu-1976-1982 msingi shule ya Nguni
1986-1987-chuo cha ufundi Yombo D’salaam kwa walemavu.
Ujuzi-welding fubluction daraja la tatu
Ukoo wangu ni lukanga kwa baba, kwa mama ni Mninda
Kuzaliwa tarehe 23-3-1963 kijiji lichehe
Kata-sindano
Tarafa-mchaulu
Wilaya-masasi
Mkoa-mtwara
Uraia-mtanzania kwa baba na mama
Kitabu hiki kiliandaliwa mwaka 1999
Mtunzi wa kitabu hikini Abeid .y.Lukanga
Cheo wadhifa mtunzi biashara ndogondogo
Hali ya mtunzi wA kitabu-mlemavu wa viungo MSAJILI WA KITABU-MCHAMBUZI-WA KITABU-MHORAJI WA PICHA –LUKAGA MWENYEWE-MCHAPISHAJI
SURA: NO 1 HISTORIA YA BABA
Baba yangu mimi Lukanga alitoka huko maheha Newala akaja sehemu moja iliyoitwa lichehe wilayani Masasi mpakani mwa Msumbij kwani kijiji hicho lichehe kiko kusini mwa Tanzania ukivuka tu mto Ruvuma kijiji cha kwanza kulikut ng’ambo ya pili ni mikomela nchini Musumbiji baba huyu alifikapale akiwa na baba yake mzee mchuluso yaani babu yangu mimi upande wa baba na bibi yangu upande wa baba alikuwa anaitwa binti mkasamba hadi ninakiandika kitabu hiki wazazi hao wote watatu wamefariki ,mzazi/mlezi niliyowahi kumuona kati ya hao ni bibi ambae nae kafariki mwaka 1976 babu upande wa baba sikubahatika kumuona na wazee hao babu na bibi walibahatika kuzaa watoto 5 na baba yangu mimi alikuwa mtoto wa 4 kuzaliwa. Kati ya watoto hao 5 wanne walisalia kuwa hai mpaka ninakimaliza kitabu hiki ni wawili tu nao wako huko mahehe newala kwa jina anaitwa binti mchuluso ambae ni shangazi yangu mimi bw lukanga kwani baba baada ya kukaa pale lichehe katika tembea yake albahatika kumuona binti hasani(SIWEMA HASAN ISMAIL) yeye aliona maisha ya upweke siyo mazuri ndipo pale alipopeleka barua ya posa kwababu mzee chilakababa wa mama yangu mimi bwana lukanga kwa bahati nzuli hakukataliwa alikubaliwa na ndoa baada ya maisha yao mungu aliwajalia kumpata mtoto wa kwanza ambayo ndo mimimwaandishi wa hiki kitabu mnamo mwaka 1963.Kwani baba yangu kaz kubwa aliyokuwa anaifanya wakati wa uhai wake ni kilimo na uvuvi wa mto Ruvuma huko mbagara na miesi na mama yangu mimi bint Hasani alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto watano kuzaliwa na kwa bahati mbaya mpaka mama anafariki mwaka 1971 aliniacha mtoto mmja tu mimi bwana lukanga tena nikiwa na hali hii ya ulemavu.
SURA 2 HALI ULEMAVU
Hali hii ya ulemavu niliipata nikiwa mtoto mdogo mwenye umri usiopungua miezi 3 baada ya kuumwa sana ugonjwa wa polio,sababu huu ulemavu siyo wakuzaliwa nao lahasha bali baada ya kupatwa na matatizo hayo ya kuumwa sana kwaani hali hiyo ya kuumwa ilichukuwa mda mrefu sana kama miaka miwili baba mama babu bibi na mjomba walihangaika sana kutaka kuokoa maisha yangu mwaka 1967 hali kidogo ikawa nafuu hapo mama ndipo alipkata tama kweli mwanangu hataweza tena kutembea kama watoto wengine na kweli hali hii ndio niko nayo hadi sasa mpaka ninaenda kuzimu
SURA YA 3 KISA CHA KIFO CHA MAMI
Mama yangu mimi bwana lukanga mwenyezi mungu alimpendelea kumpa umbile zuri hakuwa na majivuno maringo, dharau, kiburi,choyo na hasira bali alikuwa mtu wa watu kama unavyoniona mimi wmanae bwana lukanga mtunzi na mwandishi wa kitabu hiki .Kwani wakati wa uhai wao baba na mama walkuwa hawatambikii chakula ata pesa ndani ya nyumba yao aina ya chakula kama vile mpunga, mahindi, karanga,fiwi ,choroko,na ufuta vitu hivyo vilikuwa vinakutana mwaka hadi mwaka ilifikia mimi sitaki kula ugali au mboga za majani sababu mpunga na samaki ilikuwa kama unavyoona sasa mwaarabu kwa ghahawa na musuli baba yangu alipachikwa jina kuitwa (mpasula)kawachana samaki wakubwa kama vile kampango,kambare,mchali, nyigu,kaleta hao wote kutoka maji baridi katika mto Ruvumahuko eneo la Mbagara,mis na ziwa lichehe napale nyumbani watu wakawa hawapotei sababu ya kumfuata mama sababu yeye alikuwa na fai ya ususi hivyo rafiki kira siku wa nakuja kwa mama yangu mimi enzi za uhai wakempaka siku moja baba alikuwa na njaa alijalibu kumwa mbia mama apike chakula mama akasema ndio baba watoto nimekuelewa ngoja nimalize huyu dada tu nije niuwashe moto nikupikie chakula baba watoto usije ukakasirika.Baada ya kukaakama mmmda wa saalimoja baba akamtuma mwanawe aende tena akamkumbushe mama mimi nikaenda kwa mama jibu likapatikana lilelile subili kidogo mara baba akaingia ndani akachukua tenga lake akaweka nyavu sufuria,chunvi akamwambia umpe unga na kikaango nataka niende safari yangu ya mtoni Ruvuma mda tayari umesshawadia pale mama bado aliendelea kukaa tu mkoroshoni huku wateja wakimsubili atoke huyu aingie mwingine                                  


                                                      Picha


SIKILIZA VIBWEKA
Baba baada ya kula kile chakula aliendelea kurudi kula kwenye kiti chake cha kulala akamwambia mama eti namwana chukua tenga kaweke ndani mimi safari nimeahirisha mpaka kesho nimeshiba safari haiendeki mama akamuuliza kwa niniusiseme toka pale mwanzo,baba akajibu bila kufanya hivyo mke wangu chakula kisingeandaliwa mapema mimi ninaelewa kazi za kusuka bado pangebakia ngoja nimalize huyu tu huku njaa inaendelea kuuma toka siku hiyo mama nilimuona mke jasili ambayo kweli maneno ya wazazi wake waliomzaa aliyosikiliza wakati yuko mikononi mwao vilevile sijasikia kauli ya mama kumkashifu baba wala babalugha chafu kwa mama sasa sikiliza mkasa uliomkuta mama yangu mimi bwana lukanga mtunzi wa kitabu hiki na muandishi mwaka 1969-1971 huko uhongu ninaanza kukupa habari ebu tulia na usome kwa makini kipengele hiki  siyo hadithi bali ni live mama yangu mimi na mama mkubwa hawa wote walikuwa wanaitwa bint hasan sababu katika kuzaaaaaliwa  kwao walikuwa watoto watano wanaume 3 ,wanawake 2.majina ya watoto hao ni kama ifuatavyo:
          1          mtoto wa kwa nza kuzaliwa alikuwa anaitwa Ismail Hasan na huyu alizaliwa mwaka 1931 amefariki mwaka 1991
          2          Mtoto wa pili kuzaliwa anaitwa Mwanahawa  Hasaninae alizaliwa mwaka 1948
          3          Mtoto wa tatu kuzaliwa alikuwa anaitwa Siwema Hasani nae alizaliwa mwaka 1948 na amefariki tarehe 01/07/1971 ndiyo mama yangu mimi Bw Lukanga mtunzi wa kitabu hiki na mwandishi.
          4          Mtoto wan ne kuzaliwa anaitwa Abilah Hasani huyu alizaliwa mwaka 1952.
          5          Mtoto wa tano kuzaliwa anaitwa Alfani Hasani (Mdobe) nae amezaliwa mwaka 1954
Mama yangu mimi na mama mkubwa wakati huo huo walichana kila wakitembea walikuwa wapo mtu 2 hata ilifikia kuonekana watoto mapacha na wakisifiwa kujiona, unajua wakati huo kila familia ilikuwa ipo sehemu moja yaani kabla ya vijiji vya ujamaa wakiwepo na mkuu wao wa familia. Sasa ilipofikia dada yake kuolewa pale nyumbani akabakia msichana yeye peke yake, sasa Yule mama pale Mangumbu palikuwapo na mtu mmoja ambae alikuwa anamtaka kumuoa lakini mama hakuridhika na kijana yule. Pale alipofika kijana bwana Yusufu Mchuluso kutoka Maheha – Newala ndiyo mama akamkubali kijana wa pili siyo yule wa kwanza, baada ya makubaliano ya wazazi wa pande zote mbili ndipo baba yangu akafunga ndoa na mwali Siwema bint Hasani akakabidhiwa yule mwali kihalali bila utata, ndipo pale yule kijana wa kwanza aliposema neno la sikubali kumkosa Siwema kati ya watoto wale wawili wa Mzee Hasani mtoto wa kwanza kupata ndoa alikuwa mama mkubwa Mwanahawa bint Hasani yeye aliolewa na baba bw hasani Malenga kutoka Msumbiji jina jingine NAMONKONTIA basi baada ya kijana bw Yusufu baba yangu mimi bw Lukanga kujipatia yule bint waliishi kama miaka ipatayo 11 mpaka nilipozaliwa mimi nikapata akili, ndipo yule wa kwanza kutaka kumchumbia mama akaanza urasimu wa kuleta matatizo ya ugomvi pale nyumbani kwa baba. Hivyo mama yangu hakushawishika na yule bwana, yeye akaamua kuendelea kuheshimu ndoa yake bila hujali kama bwana yule ana mali nyingi! Unajua ndugu msomaji wakati huo, zamani watoto walikuwa wanaelewa wanasikia na kutii amri ya wazazi siyo watoto tulionao sasa kwani yule bwana alipoona jitihada zangu zimegonga ukuta akaamua kuleta mambo ya ajabu pale nyumbani kwa baba (Petu)
SURA 4: KISANGA CHA KUCHUKUA MPUNGA KWENYE KIKUTI (KOKWE) SABABISHO LA KIFO
Pale nyumbani petu wakati huo mtoto mdogo nilikuwa mimi tu baba alitengeneza sehemu ya kuhifadhia mazao kama vile: - Mahindi, Mpunga, Karanga, choroko na Ufuta baba aliamua kujengea kitu kinachoitwa Kokwe. Nafaka kama choroko, ufuta, kunde hivyo vilihifadhiwa sehemu za gome za miti. Siku moja mama yangu anataka kupika wali lakini lazima ukachukue Mpunga uanike ukoboe kwenye kinu, sasa ameenda kuchukua huo Mpunga yaliyokamtokea ni kama unavyoona


Picha

Baada ya kuchukua vyongo akaenda ile sehemu ya nyuma ya nyumba yetu akapiga magoti akafungua mlango wa ile hifadhi wa ule mpunga sababu pale palikuwa na sehemu 3 Mahindi, Karanga na Mpunga, kuingiza tu mkowe kuuporomosha ule Mpunga mara akaumwa na mjusi kwenye kidole cha mkono wa kulia, hata hivyo hakuwahi kweendelea na zoezi lenyewe ule uliokapatikana akauchukua mama mdogo rafiki wa yule mama  jina alikuwa anaitwa Habiba, mara mama nasikia asi mimi nikamuuliza mama je akaniambia humu ndani naona kama kuna mdudu ameniuma kidole cha kulia hivyo mkono wote naona mzito, lakini mpunga mama yako mdogo ameuanika subiri baba yako alete mboga alafu upikwe mara baba amarudi toka shamba mama mdogo akampokea jembe na pakacha


Picha


Mama ndogo baada ya kumpokea shemeji yake alivipeleka vitu alivyopokea ndani, kumbe ule wali tarari alishaupika alibakia mboga tu, baada ya muda baba alimuuliza baba mama yako yuko wapi?mimi nikamjibu mama amelala ndani anaumwa, ameumwa na mjusi wakati anachukua mpunga kwenye kile kikuti, pale baba nilimuona sura yake imejawa na huzuni, mara tukaenda wote hadi ndani kweli akamkuta mama amelala usingizi mimi nikamwamusha nikamuita mama x 3 mara mama akaitika bee baba amerudi huyu hapa. Pale mama akaamuka Akaka kitandani, hapo baba akapewa mkasa wote jinsi mama alivyoumwa na yule mjusi basi baba akasema twende kwa mzee tayari kule bondeni safari hiyo tulikuwa wote  mimi baba na mama tulipofika pale baba na mama waliingia ndani pale nikamuona baba ametoka nje amebeba vijiti vidogovidogo na kamba na dawa ya maji pamoja na majani, kufika tu nyumbani baba aliichemsha ile miti nay ale majani, baada ya kupoa akampa mama akanywa na nyingine yakufunga mkono ule aliyoumwa na mdudu, kutumia tu kwa dawa hizo kwa muda wa siku 4 mabadiliko yalianza kuonekana kwani alijitahidi mpaka mwaka akaumaliza mwka wa 2 mama akapelekwa na baba Mkomaindo kwa matibabu ya kitaalamu zaidi kule mama alikaa muda wa miezi 3 hadi mimi nikapatiwa viatu vya kutembelea (KALIPA) baada ya hapo tuliruhusiwa kurudi nyumbani mama alifikia kwa wazazi wake yaani babu na bibi huko Ulungu, napo pale alikaa muda wa miezi 2, ndipo mama alipokaomba ruhusa kwa baba yake “(mama akasema baba mimi sasa nimepona naenda nikamkute mwenzangu tukasaidiane kulima huko Lichehe) babu akasema nenda kweli mama alianza safari akasindikizwa na kaka zake wawili mjomba mkubwa na mjomba mdogo mpaka kijijini Lichehe huo ulikuwa mwaka 1971 . Baada ya kufika tu nyumbani kwake alikaa kama siku 20 homa ikalipuka upya, pale taarifa zikaja kwa baba yake, wajomba baada ya kupata ujumbe walienda kumchukua dada yao wakamleta pale huko wakiongozana na shemeji yao wakamleta pale nyumbani wakajaribu hapa na pale mungu akawasaidia akatulia, baba alipoona hali ya mwanawe safi ndipo akamuaga, babu akamuambia bibi mimi naenda kwa mdogo mke wa pili, pia mama akasema baba nenda mimi sijambo ninangoja nijitazamie nikiona hali mzuri basi nitaenda nyumbani nikamkuta mwenzangu pale tulikaa siku 14 siku ya 14 hali ikabadilika wakamchukua mpaka Zahanati ya Msikisi – Luatala Mchauru – Masasi kufika tu alipokelewa laniki matibabu yalishindikana akachukuliwa kwenye kitanda cha kamba akapelekwa kwa mganga wa jadi lakini ata huko hali ikawa bado mbaya wakaamua kumrudisha nyumbani kwa baba yake mara kidogo naona msafara wa watu wengi wamebeba machela mbele ukiongozwa na mjomba wa 4 kuzaliwa katika tumbo la mama na watu waliosaidia msafara huo wakamleta nyumbani, akafikishwa nyumba ya kaka yake mjomba ABilahi hadi ndani.

Picha

Pale ndani akiwemo bibi, baba, wajomb awote watatu wakati huo babu yuko mitala kwa mke mwingine, mama aliengesha kichwa chake miguu mwa baba huku sura yake ikimuangalia mumewe yaani baba yangu mimi bw Lukanga mtunzi wa kitabu hiki huo ulikuwa mwaka 1971


Picha


Mimi, bibi na wajomba wote 2 tumekaa kimya huku tukiangalia hali ya mgonjwa inavyokatisha tama, huku macho yetu yapo kwa mgonjwa tunamuangalia, plae nikamuona mama anainua kichwa akaita kwa sauti ya uzuni (mama, Kaka, baba yuko wapi?) wakamjibu babayako hayupo yuko Shangani kwa mama yako mdogo akarudia tena kwa sauti ya chini, mume wangu mtoto unamuona alivyoo? Atembei, mume wangu jitahidi kumtunza huyo mtoto mimi hii safari sitapona tena, huyo mtoto naomba umlee vizuri ukisaidiana na mama na kaka wote na baba baada ya dakika 3 akaniita (mwanangu mimi nikaitika nam mama Namukuu Mwanangu wito kwa mwenyezi mungu unanisubiri hivyo mwanangu bado utabaki na bibi yako babu yako wajomba zako na mama yako mkumbwa wa Sindano Mwisho wa kunukuu) Baada ya kauli ile aliangalia kwa mara ya mwisho na akaniita tena mwanangu SIJAONA, SIJAONA kwa heri (mwisho wa kunukuu) wakati haya yanatokea baba yake yaani babu mzee Hasani Ismail yupo (Chilaka) kijijini Shangani sasa wanaita Namalenga K.C.U Siku aliyokaondoka babu kuelekea huko Shangani alimuacha mwanae hali iko mzuri nay a kuridhisha aalishangaza sana pale aipofuatwa na mjomba kwani mjomba alipofika tu Namahenga akaambiwa baba hayupo ameenda huko Lulindi hivyo mjomba alipanda baiskeli hadi huko Lulindi

Picha


Kumfuata babu, mara wakakutana njiani huku babu kumbe alikuwa anarudi kuelekea nyumbani pale babu alishikwa na mshangao kipi mbona huko tofauti na siku ya kawaida huko nyumbani kulikoni? Mjomba akamuambia babu panda baiskeli twende nyumbani hali ya dada uko mbaya sana, babu akasema yule niliyomuacha yuko salama? Mjomba akasema ndiyo!! Bila kuchelewa babu alipanda kwenye baiskeli kuelekea sehemu ulikuwamo mwili wa marehemu mwanawe bi Siwema bint Hasani baada ya kufika tu pale nyumbani Ulungu babu alianguka chini na akasema haiwezekani hali hii mwanangu nimemuacha akiwa na hali mzuri sasa mnaniletea taarifa ya kifo, basi kama hivyo afadhali nimfuate mwanangu pale punde tu wazee majirani wakakusanyika eneo la msiba akiwemo mzee Mtumusha, Mzee Bilali na wengine wengi wakija kumfariji mzee mwenzao baada ya muda alitumwa mtu kwenda Sindano, Lichehe na Mgavagule kwenda kutoa taarifa ya msiba kwani ata watu wa Newala hasa Manyuli, Namahonga, Mnyava Chikunja. Baada ya watu wazima kukutana walipanga utaratibu wa mazishi muda na sehemu ya mazishi, mazishi yalifanyika siku ya pili ya tarehe 2/07/1971 saa 4:00 Asubuhi huko Shangani sasa wanaita Namalenga eneo ambalo amezikiwa mama yake babu kwa jina alikuwa anaitwa bibi bint Nang’uno

Picha


Baada ya mjadala wazee kupanga mpango wa mazishi kuwa kesho ndiyo siku ya kuzika muda ni saa 4:00 asubuhi makaburi ya Shangani pale alipozikwa bibi yake yaani mama yake babu Mzee ChilPicha
Baada ya kumaliza habari za mazishi yalifanyika kulikuwapo na tangandugu ambao walikaa pale siku 3 tarehe 5/7/1971 walimwangikana watu wa mbali kama vile Ulungu, Mgwagule, Lichehe, Sindano,Manyuli Mnyara, CHikoropora, Nagaga, Lulindi na Chitandi wote kwa siku ile waliondoka na taarifa ya arobaini ilitangazwa itakuwa tarehe 10/8/1971 kuingia kuamkia tarehe 11/08/1971 siku hiyo ya arobaini baada ya kutawanyika ndg wa marehemu walikaa wakajadiliana marehemu ameacha mtoto mmoja tena kiwete je mtoto huyu atatunzwa kulelewa na nani? Au itakuwaje bibi bint Mtumbati alisema hivyo mjukuu wangu bado nitakuwanao mimi mwenyewe hadi pale atakapopata akili mwenyewe wapi ataenda kukaa niachieni mimi wenyewe taabu atapata endepo mimi nitakufa mapema kabla yeye hajakuwa kwani akikaa kwa mtu asiemuelewa atazidi kunyongeka hivyo anastahili akae kwa mtu aliye mzoea toka awali hasa ukizingatia hali aiyonayo hayo maneno yalitamkwa na bibi yangu mzaa mama kwa jina alikuwa anaitwa Amina bint Mtumbati. Hivyo baada ya siku hiyo ya arobaini ilifikia kama siku 5 mbele siku ya 6 baba bw Yusufu Mchuluso aliomba ruhusa arudi kwao Lichehe akaendelee na majukumu mengine chakushangaza ni kwamba toka mama afariki kile kipato cha baba kilikuja kuporomoka chini ya miezi 2 ya mwanzo tu ndiyo alionekana kuwa mtu bora lakini maendeleo ya hapo mambo yalikuwa shagharabaghara ule umahiri wote wa vyakula ulitoweka na upataji mkubwa wa samaki ndo kama unavyoona mtu na moto siyo kila mara kukamata hata huduma kwa mtoto wake mimi Lukanga ilipungua Iwapo wakati huo mimi nilikuwa mtoto pekee kwa baba lakinihata hivyo niliwahi kupata lawama kumbwa kwa pande zote za wazazi.
Kuanzia kwa baba hadi kwa mama wapo walio kisema mtoto huyu hana faida sababu hana msada zaidi ya hasara kwako
Hayo yalikuwa maneno yaliyokisemwa upande wa baba (familia) na wapo waliokisema huyo baba yuko mwenyewe hakupendi kwanini ujipendekeza? maneno hayo yalikuwa yametoka upande wa familia ya mama lakini pamoja na maneno hayo yote nilichokifanya mimi kukaa chini na kutakafari hapa duniani ni nani aliesababisha mpaka mimi nikapatikana jibu nikalipata kuwa sababisho ni Baba na Mama Iwapo baba hana kitu sasa hayo yote tisa zaidi baba hata akawa kilema kama mimi mtunzi wa kitabu hichi baba ni babana mama ni mama
Kwani wapo matajiri wengi wana mali yao na pesa hawakubahatika kumpata mtoto kiwete kama mimi
Sasa mimi Baba yangu alikuwa maskini lakini amebahatika kumpata mtoto kama Lukanga mwenye fani nyingi je huyo tajiri anapokufa hiyo mali yake ni nani atairithi? Mtoto jirani baba; mama au ndugu? Mtoto na baba nani anastahili kurithi mali yake
Iwapo wote wazazi wamekufa (Baba au mama) Kwani Siku zote mzazi hawi mdogo na hawi maskini kwaani yeye ni tajiri mkubwa akiongozwa na mungu kuliko huyo unayomuonawewe (nyinyi) sababu kama ana mali nyingi kama kweli utajiri ni kitu cha urahisi jenga nyumba yahoo useme nyumba mimi nataka mtoto wa kike leo na kesho mtoto wa kiume. Hivyo ndugu zangu tusifikie wakati wa kuyasikiliza maaneno ya nje ambayo yanaleta mfarakano katika familia mwisho mtaachwa gizani haujui wapi uelekee, kwani mimi bila kuwa na akili ya kufikiri ata sehemu nyingi nisingezijua kilichobali bado ningekuwa mlemavu wa jochoni kama giga halitoki, au huonekana mpaka siku ya kubomolewa nyumba siku ya kubomolewa nyumba tuache akili potofu na kuengemea upande mmoja wa kuzaliwa, kwaani mtoto ni wa pande zote mbili umemina ukemi. Kwaani mimi nimeweza kupata zawadi za watoto watatu 3 lakini hayo yote yametokana baada ya kuwa na uvumiivu na ubusara ndiyo maana mungu nae alinipa msaada wa kufanikisha kuacha kumbukumbu hapa duniani ya watoto.


SURA 5: ELIMU YA WADUDU

Elimu ya wadudu ambayo sasa tunaita awali nilianza mnamo mwaka 1974 chini ya mwalimu? Bilali na Cozimo katika shule hiyo mlemavu nilikuwa mimi peke yangu kwaani ata hivyonilikuwa ninajisikia vibaya sana kutokana na hali niliyonayo mungu alinijalia kunipa kipaji cha kuele mapema nilisoma shule hiyo ya vidudu ndani ya miezi 3 tayari muelekeo wa kujua kusoma ilipofika mwaka 1975 mwezi 6 nikawa tayari minapambana vizuri kusoma, mpaka nikapata cheo cha kuwaandika wanafunzi wanaotia fujo na kelele darasani wakati tusiokuwa bado kuandika vizuri tulikuwa tunaandika chini, mpaka mwaka 1975 walichaguliwa wanafunzi wengine kwenda kuanza shule ya msingi huko Lulemba Luatala kama vile wanafunzi :- wafuatao Habiba, Omari Mzee Omari, Hasina Hasani, Juma Huseni na wengine wengi. Pale tulibakia na wanafunzi wafuatao Ahmadi Mbaga, Asumini Hasani, Biena Rashidi, Exsevia Chikodi, Zawadi Mpelembe, Dorose Ngaeje, Veronika Luka na wengine wengi pamoja na hesabu hiyo wengine wanatangulia ukumbi na haki.

SURA 6: ELIMU YA MSINGI

Elimu ya msingi nilianza tarehe 1/1/1976 katika shule ya msingi Nguni Chini ya Mwl. Mwanzilishi Isca Masudi kutoka Mnyambe Newala huyo alikuwa mwalimu wa kwanza kuja kuanzisha na kufungua shule pale kijijini Nguni Kata ya Sindano Tarafa ya Mchauru Wilayani Masasi yeye alikuwa mwalimu Mkuu wa kwanza. Orodha waalimu:-
1.      Mwl. I. Masudi 1976 M/ Mkuu
2.      Mwl. E. Ng’andile 1977 M/Mkuu msaidizi
3.      Mwl. M. Zaburi 1978 – upe
4.      Mwl. H. Sadiki 1978 – upe
5.      Mwl. V. Samuel 1979 – upe
6.      Mwl. J. N. Nchimbi 1979 – upe
7.      Mwl. M. Yasini 1979 – upe
8.      Mwl. J. Kaondo 1980-upe
9.      Mwl. O. Abdalah 1980 –Chuo
10.  Mwl. J. Kungunda 1978 – upe

Katika walimu hao wengine wapo na wengine wametangulia kwa mwenyezi mungu atahivyo naomba tuwaombee mema na maovu yaondolewe. Mwaka 1979 palifanyika mabadiliko Mwl. Masudi alihamishiwa Luatala (Lulemba) na Mwl. M. Kyando alihamishiwa katika shule ya Ng’uni kayika waalimu hao mwlKipando ndiyo alikuwa mwl. Mzuri sana kwa ufundishaji alifuatiwa na mwl. J. Kaondo huyu kaondo somo ambalo alikuwa ana stadinae ni somo la English na Sayansi na Mwl. Kyando yeye alitisha kwa masomo yafuatayo Hisabi, English, Historia, Sayansi, na Geografia ni mwl. Ambae elimu yake ukiisikiliza utafika sehemu mzuri kwanza alikuwa mkali kama ulivyokimuona Rais che Mkapa yeye alikuwa hataki kucheka au masihala na wanafunzi kila wakati. Pia masomo yake alikuwa anapenda kutoa test kila siku ya Jumatatu, Jumatano, Ijuma na Jumamosi maswali yake yalikuwa siyo chini ya 50, 45 na 35 na alikuwa anakubali kununua kipindi ili aingie yeye darasani.

SURA 7: WADHIFA – SHULENI

Wakati niko shule ya msingi darasa la II niliwahi kushika nafasi ya kufundisha wanafunzi wa darasa la 1 vilevile mimi kutoka darasa la 1 nilikuwa mwanafunzi pekee ninayojua kusoma darasani Na nilikuwa catibu wa kamati ya EK ya shule kusimamia miradi ya shule na muuzaji mkuu na mnunuzi wa mali na vitu vya shule
Kama vile ule mikorosho ya pale shule ya msngi Ngumi ambayo ilikuwa imeuzunguka eneo lile lote hadi kule kwenye uwanja wa mipira ile yote ilinunuliwa na mimi Lukanga na Monika Ausi Rehema Manuweli na AHMADI Mbaga kwa thamani ya 15.00.Watu wengine wanao kifahamu kijiji cha Ngumi barabara ya kutoka Masasi kawe unaelekea Newala utafika kijiji cha Mbuyumi pale utaelekea upande wa kulia utafika hadi shamba la bibi (Msifu akiba)kijiji cha kwanza kutoka Mbuyuni







PICHA
  



Utoka ngumi unafika msikisi kachulu ndiyo umefika kijiji kongwe Luatala alipotokea marehemu saad kwani alifika pale enzi ya utumwa akiwa na umri wa miaka saba toka Omani biashara yake kumbwa ilikuwa uuzaji mayai ya kuchemsha mpaka akafkia kuwa tajiri akiungana na Waarabu wenzake.
Pamoja na taarifa hizo shuleni niliwahikuwa mpinga  filimbi mkumbwa wa bendi ya shule Pamoja na habari hizo  za shule ya msingi bado niliendelea kuwa mwanafunzi mwanye upeo wa akili darasani nilikuwa shule ninaipenda iwapo sikuwa na usafiri wa kutembelea kwani kutoka nyumbani hadi kufikia eneo lililokuwepo shule kulikuwa kama umbali wa mita 175 hivi nawakati huo



Picha





ninasoma siyo mufikirie kama nilikuwa natembelea baiskeli kama mnavyoniona hivi sasa la hasha, wakati mambo ya baiskeli ya tairi tatu kwangu ilikuwa kama muuzaji wa Gongo na polisi yaani (sumu) hamna. Wakati nipo darasa la Saba chini ya Mwl. Mkuu Dokta M. Kyando Mkinga toka Iringa tuliwahi kufanya mitihani ya kata shule 5 shule zenyewe ni hizi zifuatazo;-
(1.) S/M Luatala
(2.) S/M Ngwagule
(3.) S/M Sindano
(4.) S/M maparawe na
(5.) S/M Ng’uni
ambayo nilikuwa ninasoma mimi bwana Lukanga baada ya mashindano hayamimi nilishika nafasi ya saba (7) kati ya shule hizo tano (5), ndugu msomaji unaposoma habari hii usifikirie kama taarifa hiyo ninajipendelea hapana, wapo wanaonifahamu mimi wakati niko Shule ya Msingi mimi nilikuwa ninakifanya wakati niko darasani kati ya waalimu wanaofahamu habari zangu wakati niko Shule ya Msingi Ng’uni kuanzia mwaka 1976 – 1982 ni mwl Mauridi Yasini sasa amestaafu yuko hapo Mkangaula tarafa ya Lulindi Mwl. Mkulia yuko TTC Chuo Cha Ualimu kwani yeye alifika pale kumfuata dada yake Mwl. Adija Hokororo ambayo aliolewa na Mwl. Abdalah ambayo alifariki kwa ajali ya kuumwa na nyoka huko shambani Ulungu, wengine wanafunzi wenzangu ambayo tulikuwa yunasomanao darasa moja kama mama niki anayoishi Mtwara Ligula B Rehema Manyela Costantasi mwembe yuko Dar-es-saalam na wengine wengi wanaonifahamu mimi Abeid Yusufu Lukanga Na wakati niko nyumbani kama vile siku ya Jumamosi na Juma pili nilikuwa napenda sana kusoma vitabu vya hadithi kama safari ya Bulicheka, Abunuasi, Halfu lela Horera, wile gamba na Shabani Robart. Pamoja na vitabu vya Historia ya Mtanzania alivyoteseka na maisha ya utawala wa kislutani na wadachi wakati wa ukoloni hadi sasa babu zetu wengi wamepoteza maisha yao huko marekani, uingereza na wengine bado wapo huko njee ndo wale unaowasikia wamerekani weusi utundu niliyokawanao laniki ikifika wa usiku nilikuwa ninajisomea iwapo wakati huo mafuta ya taa yalikuwa siyo watu watu walikuwa na uwezo wa kuyatumia lakini mimi nilisoma kwa kutumia moto ndiyo ninasoma kwa kutumia mwanga wa kuni (moto)

SURA 8: MAISHA YA KUWINDA NDEGE

Ndugu mosmaji pamoja nilikuwa na hali ya ulemavu (kiwete) sikujiridisha nyuma mambo ambayo nilikuwa ninapendelea wakati huo enzi ya utoto wangu na ujana ni kucheza mpira wa miguu mimi nilikuwa natumia kucheza na kupiga kwa mikono hasa nilikuwa napenda kukaa golini kwa kweli kama vile shuti la kimo cha ndama wa ngo’ombe, mbuzi hapo nilikuwa ninaruka kama ninaruka kama unavyomuona chura anavyoruka wakati wa kutembea kwake kwa kweli ukinikuta niko na mpira kule golini wewe mwenye utapenda mambo yangu.

Picha






Pamoja na zoezi hilo la kuufanya mwili uwe katika hali zuri ya kukaa sawa vilevile nilikuwa napenda sana kutengeneza vizizi vya ndege kama vile: - Chiriku, Mbilingo, Kunjeni, Kidididi na ndege hao nilikuwa ninawafuga mimi mwenyewe hasa nilikuwa ninawatega kwa kutumia ulimbo na madema

Picha





hapo ninatega mitego ya kaga, kerengende, deya na kware chambo Mtama na Mahindi ndugu Msomaji shughli hizo zote wakati ninafanya bado niko hali hii ya ulemavu wangu.Pamoja na utundu wangu wote nilikuwa nakumbana na matukia mengi sana kama manyigu na kushika kinyesi cha watu waliokuwa wanajisaidia porin.


SIKILIZA VITUKO PORINI
Siku moja jumamosi nilibeba mfuko wangu na filinyongo na manati yangu nikaenda Porini hatua sana na nyumbani yetu nilipofika kichaka kimoja kuangalia juu nikawaona ndege njiwa (deya wawili) wamekaa sehemu moja huku wakipeana lomasi za kimapenzi huku bila kuelewa kuwa hapo chini kuna mtu anawatafuta ndge hao wanaojizuka na hisia ya mapenzi porini loo punde si punde nikachukua silaha yangu manati nikaweka risasi inayofanana na ndege wale wote wawili kwa kweli ndugu msomaji wakati huo bwana Lukanga usimtoe kwenye kitu nikachoitwa manati kwake nilianda  bunduki na risasi nikamuangalia ndege amekaa wapi nikawaona nikatanua manati nikaachia virinyongo bila hajizi ikatua kwenye kichwa cha ndege mmoja, huku akifanya jitihada za kuanguka chini, akakutana na ghaidi nyoka mkubwa kufika tu pale kwenye nyasi akabanwa na yule nyoka, mimi nikienda kumuokota namuona nyoka amembana yule dege mdomoni, sasa pale nikasema nyoka kama huyu akiniuma mtu kama mimi nitaweza kweli kukimbia mpaka nyumbani? Palepale mungu akanipa ujasili nikachukua manati yangu kama kawaida yake nikamtafutia risasi inayofanana na nyoka yule nikaipeleka eneo la kichwa, mara moja yule deya akamuachia chini yeye akaanza kumtafuta adui yake aliyemsababishia akose kitoweo kizuri siku ile huku akielekea nikiko mimi, na mimi kukimbia siwezi nikampa manati ya pili pale pale bila kuchelewa na mawasiliano yakakatika ya ukali wake muda huo nikaamua kurudi numbani bila kitoweo chochote kile huku nimenyong’onyea, kwani kufika tu nyumbani nikamkuta mjomba anagoma kuhusu mimi kutoka nyumbani asubuhi kwenda porini mbali peke yangu, Bahati mzuri toka nizaliwe mjomba yangu hajabahatika hata siku moja kushika fimbo au kunyanyua mkono wake kunipiga. Pamoja uandike habari iweze kuwa na chumvi sukari ili iinoge hapo siwezi mjomba (wajomba) zangu kuwapatia lawama la kunipiga lakini pamoja na vituko hivyo vyote vya maporini, nilikuwa sisahau kamwe kusoma na toka nianze shule sijakosa shule kwa ajili ya uzembe bila taarifa ya mwl. wa Zamu au mwl. wa dasara unajua hiyo ilitokana na msimamo wa mojmba yangu kuwa mkali juu ya mimi nipate elimu ambayo hapo baadae nitaweza kuvumbua mambo ya ulimwengu kama huu uandishi wa vitabu ningekuwa shule nimezembea je haya yote ningeyaweza wapi? Ukiona shule siendi ujue siku hiyo ninaumwa na lazima taarifa nipeleke kwa mwl. wangu wa darasa na mwl. wa zamu kwa siku ile.

SURA 9 KISA CHA KUTAMBUA MAMBO MENGI YALIYOTOFAUTIANA HALI YANGU YA ULEMAVU

Pamoja na hali yangu ya ulemavu wakti huo niliona kuwa hawa waliopewa madaraka ya kunitunza mimi wkati huo niliwaona wananionea sana sababu vitu waliokuwa wananipa kufanya vilikuwa tofauti sana na uwezo wa hali yangu kiutendaji kama vile kulima shamba kukafua mtama, kunde, uwele, mbaazi, kupika ugali wa Mtama, mahindi kwani babu yangu alinitengenezea kinu cha kwangu cha kutwangia Mahindi, mtama, hayo yote niliyaona kama ninaonewa wakati kumbe kote kulikuwa kufundishwa maisha ya upweke jinsi ya kuishi kama ilivyo sasa baba, mama na bibi wote ndiyo viungo wakuu kwa mtu kama mimi sababu sikubahatika kuwa na pesa za kuweza kunilinda siyo chini ya miaka 5 mbele maisha yenyewe yakubahatisha leo ndiyo kesho hapana. Baba yangu mimi hakuwa na uwezo wa kutosha kwangu kwanza alikuwa mkulima mdogo na msusi wa mikeka na majamvi vitu hivyo ndio vilikuwa vinampatia riziki ya kuweza kuishi kitu kikubwa kilichokamsaidia sababu alikuwa maisha ya vijijini siyo mjini nyumba yake siyo ya kupanga. Wakati niko darasa la IV baba yangu aliona afadhali huyu mwanangu kwa kupunguza ghasia ya huduma afadhali nimkabidhi kuku wawili dume na jike kusudi wakiwa wengi wamsaidie kwenye huduma ya shule kweli mungu alisikia kilio chake kuku walizaana wakafikia 23 watano wakashikwa na mbweha waliosalia wengine niliwauza nikapata pesa ya hulipa ada ya shilingi 100 kwa miaka 5 @ sh 20/= na pesa zingine nilinunua uniform na sabuni, wakati huo tulikuwa tunatumia chini kaki juu nyeupe kwani pamoja na hayo maisha yangu yalikuwa ya chini sana ilifikia kutamka maneno kwa nini akutoweka baba ili mama akabaki? Sababu ya maneno hayo yalitokea wakati wa mchana saa 6:00 mapumziko nilikuwa sirudi nyumbani kuogopa jua kwani nilikuwa naumia sana kwani magoti na mikoni (viganjani) hivyo nikawa ninaamua kukaa mpaka muda wa kutewanyika huku nikifika nyumbani ninkauta ugali wa mhogo umevaa oti na ndugu yake kisamvu pale nikkimaliza kula ninapata kazi ya kufanya kama vile kukafua mtama au kazi yeyote ile ilitegemea na siku yanyewe, lakini mimi sikuona vibaya kwangu.

SURA 10: KUMALIZA ELIMU YA SHULE YA MSINGI

Mwaka 1982 kumaliza shule ya msingi kwa bahati mbaya shule yetu hakuchaguliwa mwanafunzi yeyote yule kendelea na masomo ya sekondari na sisi ndiye tulikuwa wanafunzi wa kwanza kufungua LY 1982 chini ya Mwl. Mkuu Dokter M. Kyando, baada ya kuhitimu masomo ya msingi niliamua kujishughulisha na kilimo kidogo na biashara ndogondogo kama vile uuzaji wa korosho za kukaanga na sigara mwaka 1983 niliamua kwenda kwa mama mkubwa huko kijijini Sindano II baada ya kufika pale kijijini Sindano nilifika na pesa tasilimu sh 80/= pale nikajishughulisha na biashara ya sigara, ndizi za kuiva na kujifundisha usukaji kofia, mkeka, kambaa, makapu na majamvi mwalimu wangu wa shughuli hizo alikuwa dada Fatuma ambaye ni mpwa wa baba mkubwa pale kwa mama mkubwa nilipofikia na rafiki yangu mpendwa bwana WANYENGA kwa kweli kufuatana na ujasili wangu wa uelevu kazi hizo baada ya kufundishwa mimi sasa niligeuka kuwa ndiyo fundi mkuu pale. Mwaka huo 1983 mwezi wa tatu Mwl. Kyando aliamua kuniita niende pale shuleni Ng’uni ili nikarudie darasa la sita sababu Mwl. wangu Mkuu hakuridhika mimi kukosa kuingia kitado cha kwanza lakini mimi sikupendelewa na uamuzi huo kitu nilichokakiona ni siku ni siku ile ya mtihani kutolewa kwenye chumba cha mtihani sababu kule kote walikuwa wananifahamu jinsi hali ilikiwa wakati niko class hata hivyo nilienda kuanza darasa la sita mwezi wa tatu tarehe 06/3/1983 wanafunzi tuliokawanao ni mwl. Mkulia sasa yuko hapo T.T.C Mtwara Joseph B. Nichelewa, Andrew Bunaya, Hasani Issa na wengi baasi baada ya kufika tu pale darasani mwl. Nilimuambia siku hiyo ikifika ya mtihani hapatatokea kasheshe? Mwl. akasema mambo yote nitayarekebisha mimi, ndipo mimi nikaenda tarehe 6/3/1983. Wakati huo ninafanya prosesi ya kuripiti nilisikia tangazo kwenye Radio ya Taifa kuwa kuna Chuo Cha watu wenye ulemavu kiko Yombo Dar es Salaamu anwani yake, mimi nikafanya ajizi niliandika barua kwa kutumia anuani hii


Kulia – Mwaandishi
MR. ABEID Y. BOMBA LUKANGA
C/O P.O. BOX 43
LUPASO – MASASI – MT
Kushoto – mpelekewa:-
CHUO CHA UFUNDI YOMBO
S.L.P. 49006
DAR ES SALAAM.

Barua hiyo baada ya kuiandika majibu yake yalifikiwa kwa mkuu wa chuo cha vipofu pale Mtapika wakati huo yeye nalishikia kofia 2 Afisa Ustawi Wilaya na Mkuu wa Chuo kwa jina alikuwa anaitwa KAPEPETA majibu yalibidi mpaka mimi niende mpaka Masasi kwa Afisa Ustawi wa Wilaya ambayo ndo huyo Mkuu wa Chuo pale Mtapika ili niende Hospitali ya Mkomaindo ili nikajaze fomu lakini nitarudi nyumbani, mwalimu wangu aliniruhusu, safari ikaanza kutoka Ng’uni kuelekea Mtapika tulifika siku ya tarehe 23/3/1983 Mtapika tulifika saa 9:30 alasiri baada ya kunipeleka mjomba aliambiwa aniache mimi nitarudishwa pale mambo yatakapokuwa tayari kweli pale Mtapika nilikaa kama miezi 4 nikarudishwa nyumbani Sindano tarehe 13/7/1983 kwa kweli sababu kule nilikaa sana hivyo ule mpango wa kuendelea na shule haukuwezekana hivyo nikaamua sasa kujishughulisha na zile biashara ndogondogo kutembea kwangu na kuishi na wale vipofu pale Mtapika ndiyo kulikonifanya niwe mwaminifu wa vitu vya watu hasa ukizingatia wale walikuwa watu ambao hawaoni hivyo mungu alinipa mtihani mkubwa, kwani pale kijijini Sindano niliweza kuishi maisha ya ustaarabu na kushindana na watu wa kawaida mpaka nikajenga nyumba mwaka 1985 kwa gharama y ash 387. 00 na mjenzi wa nyumba hiyo alikuwa Bwana ANTON MAHUNDU kwani nyumba hiyo sikupata msaada kwa ndugu zaidi ya kaka yangu Mzee E. KAZIBURE ambayo alinipa mlango ambayo niupeleke kwa fundi Mzee Laisi Sindano ya kwanza mkombero kwa gharama y ash 150/= tarehe 22/2/1985 niko katika shamba langu huko bondeni sehemu moja inaitwa Lukwika kijimfereji kimoja kidogo nilimuona mdogo wangu Bwana Ibrahimu H. Malenga ananiambia kaka Mzee Kazibure ameleta barua yako, nikiangalia kwenye stamp ninaona muhuri wa Dar es Salaam baada ya kufungua ndani nikakuta majibu na Chuo cha Ufundi Yombo Dr es Salaam, kwa kweli nilifurahi sana palepale nikaacha kulima nikaanza msafara taratibu wa kuelekea nyumbani nikatulia nikaisoma kwa makini barua ilikuwa inasema hivi nanukuu.
Ndg Abeid Y. Bomba umechaguliwa kujiunga na Chuo Cha Ufundi kwa walemavu Yombo Dar es Salaam kuanzia tarehe 06/01/1986 unahitajika kuwahi mapema kabla nafasi aijajaa vilevile unahitaji kuja na vitu vifuatavyo:-
1.      Godoro 1
2.      Neti 1
3.      Shuka 2
4.      Kaptura / suruari 2
5.      Daftari 10 kubwa
6.      Peni na penseli 10
7.      Shati 2
8.      Beg au sanduku
9.      Nguo za kubadili
10.  Overroli 2
11.  Nauli jigharamie kama kutakuwa na utata wa usafiri toka hapo ulipo hadi hapa Dar es Salaam mwisho wa kunukuu. Baada ya kupata barua hiyo nilijaribu kukusanya wanafamilia ili yule alichonacho aweze kukitoa.
Lakini siyo haba mwenye uwezo wake pamoja na taarifa nilipeleka kwa baba mzazi Mzee Yusufu Mchumbo iwapo alikuwa hana uwezo yeye pekee pamoja na shughuli zake za usukaji mikeka aliweza kunipatia pesa tasilimu sh 400/= wakati huo hivyo nipesa kubwa sana, ata hivyo kwa sababu mimi mwenyewe nilikuwa ninafanya vijibiashara ndogondogo baada ya taarifa hiyo ya safari ya kwenda Dar es Salaam kusoma mimi mwenyewe nilikuwa na pesa tasiliku sh 800/= hivyo mpaka ninaanza safari pale kijijini Sindano II Ng’uni pale ndipo msafara ulianza rasimi hiyo ilikuwa mnamo tarehe 28/12/1985. Mjomba MDOBE IV ndiyo aliyokanichukua kutoka Nguni k.c.u hadi Masasi kwa baiskeli aina ya swala. Masai tulifika majira ya saa 6:15 jioni akanipeleka hadi Mtapika Chuo Cha Vipofu wakati huo Mkuu wa Chuo alikuwa Mzee Kapepeta, pale Mtapika tulifika kama saa moja usiku tulipokelewa vizuri sababu mimi sikuwa ngeni wa mazingira yale, mimi nililala pale bwenini na wanachuo na mjomba alienda kulala nyumba zza wafanyakazi, asubuhi mjomba alikuja kunichukua hadi stand Masasi Mjini kufika tu basi la Iddis au Joka Jagwa busi hilo lilikuwa linalala Lulindi na kuja hadi Nagaga – Masasi kuelekea Mtwara wakti huo kutoka masasi hadi Mtwara nauli yake ilikuwa sh 90/= tu.



Picha





Huo ndio msafara wa Masasi – mtwara kwa Bus la Joka Jangwa ilikuwa mwaka 1985.
Baada ya mjomba yangu kunisindikiza pale stand alipoona mwanae tayari amepanda bus yeye alianza safari ya kurudi nyumbani ng’uni. Msafara ulianza Masasi hadi Mtwara, Mtwara tulifika majira ya saa 11:30 jioni kufika tu stand kubwa Mtwara baada ya kuteremka tu kwenye lile bus nikakutana na bwana mdogo Josefu B. Nichelewa ambayo yeye alikuwa anaenda kwa baba Mzee R. Nichelewa ambayo huyo baba alikua anafanya kazi katika Ofisi ya CCM Mkoa walikuwa wanaishi pale Majengo Vitus nyumba No 6 karibu na Kasisa la MAjengo kwa father Idifons, pale nilikaa kama siku 4 siku ya tano akanichukuwa bwana mdogo Isca nichelewa kwa baiskeli hadi Ustawi kwenda kuchukua tiketi ya meli ya MV Lindi safari ilianza Mtwara – Dar es Salaam ilikuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 6/01/1986 wakati huo nauli ya meli ya MV Lindi ilikuwa sh 85/=

Picha






Hilo gari ndogo ni alilokitumia baba Mzee Nichelewa la CCM Mkoa na dereva wa gari hilo alikuwa Mzee Mchunga ambayo watu hao wote wameshatangulia katika ukumbi wa mwenzi mungu kwa hiyo gari hilo ndilo lililonichukua pale Majengo hadi Bandarini, kwani hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kupanda meli, kwani safari hiyo nilipata shida sana yale mawimbi ilisababisha kutapika kila mda mpaka chakula chote nikakitoa kwani mle ndani ya meli nilibahatika kumpata rafiki wa kike ambaye yeye alininunulia chakula chochote kile tu nilichokitaka pamoja na hayo ilikuwa bure tupu, kwani niliyofanya kazi ya kulala toka siku ya Jumamosi hadi usiku wa manane tulipokutana na meli kubwa sana wakati huo meli yetu ilikosa muelekeo haku  na mawasiliano ya tunakotoka wala tunakoenda ile siku ya pili yule rafiki yangu aliniamsha akaniambia Darling angalia Matank ya kule kigamboni. Hellow mpenzi ebu amka sasa tuko karibu kufika Dar es Salaamu niliyafumbua macho yangu na kuangalia huku na kule nikaanza kuona minazi, matanga nay ale majumba marefu ya pale Kilimanjaro Bongo mweneti tulifika majira ya saa 11:05 asubuhi.

SURA 11: MWANZO KUINGIA JIJI LA DAR ES SALAAM (BONGO)
Loo Mwenetu kweli Bongo ni jiji la kushangaza kwa Mgeni anayotoka sehemu yoyote ile ambayo vitu na raha zile haziko kwao alikotoka, kwa kweli lazima upagawe na usipoangalia na kuwa makini utakuwa chakula cha Simba (GARI) ndugu Mshirika kufika tu bandarini niliteremka tukaenda hadi pale kibandani yaani mapokezi kwani msafara wetu wa kuelekea huko chuoni jumla tulikuwa wnafuzi tupatao 6, wanafunzi 4 tulikuwa wa mwaka wa kwanza na 2 mwaka wa pili, pale sababu wenzetu wlaikuwa wenyeji wao walituacha solemba sisi pale tukabaki washamba tupu, lakini afa hivyo sababu mimi nilikuwa na yule rafiki yangu wa kike alinisaidia kwa kunipa mawazo jinsi ya kufanya utaratibu wa kufika Chuoni Yombo, tukajaribu kupiga simu, simu inaingia kutoa no, mwisho kale kapenzi kangu akaniambia hapa lamsingi nikuchukua Tax tu Bandarini – kiwalani Yombo lakini nauli yake ni kubwa sababu kule madereva wengi wanakataa Yombo sababu kuchafu nauli yake itakuwa sh 10 au 15 basi sikuwa na ujanja ikabidi nitumie uamuzi huo, tukaita tax moja akalewana na yule rafiki yangu wa kike ambao yeye akaanza safari kazi kubwa ilikuwa kuliangalia jiji la Dar es salaam (Bongo)kama linavyotamkwa sifa zake na wale waliowahi kufika na magazeti, redio, na sinema kwa wakati huo, ndipo pale nilipokubali kweli hii ni Bongo au Dizim ukifanya isivyo utarudi jina, kwanza niliyoona magari mengi, watu majumba kama wadudu siafu watafutapo chakula, mara tukakona pacha ya Vingunguti kwa kuelekea kushoto barabara ya uwanja wa ndege Nyerere Road tukaacha mbele safari moja moja mpaka GV group tunaipita tukafika Bom Bom tukakunja kushoto hadi darajani tukaacha Baa maarufu sana wakati huo ilikuwa inaitwa TUMAINI BAR ambao lilikuwapo na bwalo la muziki. Tukakona kushoto tukafika Geusti ya Bushoja na Nyanza geusi House tukafika getini asikari alifungua geti tukafikishwa mikoroshoni, sababu Chuoni petu palikuwapo na mikorosho mara tukasikia mabwenini walete hao waje wale maharage na dagaa.Dereva baadaya kwenye beg langu nikachukua pesa sh 15/= nikamlipa baada ya kulipwa ile pesa dereva alituaga akasema ndugu nzangu ahsante mungu akipenda tutazidi kusaidiana nasi kwa pamoja tukasema ahsante sana by by, kwaani dereva tulimshukuru kwa kutufikisha salama bila kutuongezea ulemavu mwingine , vile tulifika wkati muafaka wa chakula , bila ajizi sikujichenga wala kuona aibu sababu pale pote tuko walemavu tupu wa kila aina kuhiwapo na watu kama mimi Lukanga mtuzi kama kitabu hichi na maalubino vizuri kama vile esta Chikoti dada ambayo anakaa pale kwenye uwanja wa Ofisi ya Magereza nyumba ambayo iko karibu na mishondo, kwani dada huyu mama yake alikuwa anaitwa bibi Shola na sasa bibi huyo ni marehemu kwa ajali ya gari nilipoingia mle ndani mesini nilikutana na rafiki yangu mmoja kwa jina anaitwa Hamisi S. Nankoma kutoka Luagala, kwa hiyo wote tulitoka huku kusini hasa Lindi na Mtwara letu lilikuwa moja akaniambia mbwauwa moja akaniambia tukale sembe, mimi sikujichenga niliingia bwaloni nikaufinya ubwabwa kwa maharage, pale chuoni petu tulikuwepo jumla ya wanafunzi wapatao 200. Mimi baada ya kufika tu nilipelekwa bweni la MKAWA  pale nilikaa muda wa siku 15 sababu bweni hilo la Mkwawa lilikuwa na na shida ya maji hivyo nikahamishiwa bweni la Sokoine huko nilikutana na Mzee Sakaragha, Mzee Mchopi hayo yalikuwa majina ya Utani.                                                                                                                                                                                                                                               

SURA 12 BW LUKANGA KUANZIA DARASANI KUTAFUTA FANI INAYOMRIDHISHA
Katika chuo chetu kulikuwa na jinsia zote mbili yaani Me na Ke utaratibu wa pale ulikuwa ukifika wakati wawanafunzi nusu ya idadi inayohitajika ndipo pale mnaingia darasani fani zilizokawepo chuoni pale ni sita nazo ni kama zifuatazo:-
1.      Ushonaji (nguo)
2.      Ushonaji (viatu)
3.      Useremala
4.      Kilimo
5.      Tay pist
6.      Welding (uungaji)
Kumbe sheria za pale ilikuwa ukifika tu darasani wiki 2 za kwanza unapitia kila fani ili kukuangalia je huyu na ulemavu wake fani gani anaimudu?. Mimi nilipendezewa sana na fani ya UUngaji vyuma ambayo mwl. Wetu alikuwa anaitwa Mwl. Kipengele Mndengeleko toka Rufiji ndugu msomaji mwalimu huyo iwapo alikuwa na matatizo ya akili. Ilikuwa fani hiyo ya uungaji inamuafiki sana, yeye alilala sana upande wa vitendo siyo Nazaria ndugu msomaji fani ile ilinisumbua sana siku za mwanzo, lakini baada ya uzoefu mambo yalikuwa bomba mnamo mwaka 1987 aliletwa mwl. Wa kike toka Chang’ombe kwa jina alikuwa anaitwa mwl. Mabula (msukuma) yeye aliletwa kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya nazaria na vitendo, yeye alifundisha sana nazaria ili fundi chuma ufahamu umbile la chuma na ukifahamu chuma (aina) kwa kuchoma, kukata, kutoboa na kukereza. Kwani baada ya kufika pale chuoni niliwakuta wanachuo wengi wanao baiskeli ya tairi tatu, hivyo yule rafiki yangu Bwana Haisi alinionyesha mbinu nyingi na sehemu wanazoweza kutoa msaada wa hizo baiskeli kama vile:- Tazara, Scanic lion club, rotali club na mwanamboka sevisi wakakti huo sikumoja pale chuoni petu walifika wa hindi kuja kutoa msaada wa chakula pilau biliani maziwa kwa muda wa wiki 2 mchana na jioni, vile vile walitoa anuani yao kama kunamtu anayotaka kuomba msaada tunamsaidia iwapo shirika letu limekuwa dogo mimi nilikuwa mtu wa mwisho kupeleka barua katika ile sehemu yao sababu pale mahali mimi katika mzunguko kupaona katika msikiti wao barua niliandika tarehe 9/5/1986 majibu nilikuja kujibiwa tarehe 16/05/1986 siku ya Jumamosi na tarehe 17/05/1986 ndiyo siku walikuja kunichukuwa wao wenyewe wahindi hadi mfawa India Ghandi, kufika pale nilikabithiwa baiskeli mpya ya tairi tatu muda wa saa 9:15 alasiri.

Picha




Na baiskeli hiyo ndiyo hii ni hiyo nayo hivi sasa wakati huo sh 17,500/= toka kiwandani sido pale Dr es salaam inauzwa sh 700,000kwani kupata tu kwa baiskeli ilikuwa ukombozi tosha wa maisha yangu.

SURA 13: KUMALIZA CHUO TAREHE 3/10/1987
Baada ya kufanya mtihani wa Taifa wa chang’ombe mwaka 1987 matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:-
(1)   Nadharia C
(2)   Vitendo B
Tulifanya maafari ya kuhitimu mafunzo, palikuwa na sherehe ya mziki watu walicheza kama siyo vilema, wenye kunywa walikunywa waliokalewa walikuwa chakali kama unavyomuona kenge anavyofukuzwa na mbwa, lakini hayo yote kamaunavyoelewa hakuna asiyependa kushindwa kufanya mambo mengine siku ile ya sherehe asubuhi yake watu waliandaliwa tiketi ya kwenda makwao, idadi ya wanafunzi tulikuwa 250 wengi walikuwa wa mwaka wa kwanza, ndugu msomaji chuo hicho ndipo kilichonifumbua macho na kujua jinsi mlemavu avyoweza kuishi maisha ya upweke bila kuwa tegemezi kwa mtu kila muda, sababu chuoni pale hakuna baba, mama wala shangazi jibu unapata hakuna kubweteka. Baada ya kuanza safari mimi nilipanda bus stand ilikuwa pale kisutu baada ta kufika hapa Mtwara niliteremka pale polisi nikachukuwa ile baiskeli ya tairi tatu hadi ofisi ya ustawi wa jamii wakati huo afisa ustawi alikuwa ndugu Mkilanya, pale nilipokelewa na kutoa barua inayotoka chuoni ya kuwakilisha kweli huyo mwanafunzi amehitimu mafunzo ya ufundi miaka 2 Afisa Ustawi mwanafunzi alimpeleka Nandope guest house pale nilikaa muda wa siku 14 siku ya 15 nikasafirishwa hadi Masasi kwa bus la Mtwadeka kwa kutumia warrant siyo siku hizi mlemavu unajitegemea, lasivyo unatupwa (kuteremshwa popote pale) bila kujali kama mlemavu ulemavu mzazi wako ndo anayejua hali hiyo kondo au mwema sasa siyo ule dunia ya watu wa sasa siyo ule wa enzi ya mwl. J.k. nyerere Bunto watu wlaiopo sasa wako katika kutegeneza vitambi vyao siyo kujali hali ya wananchi wao ndo maana sasa uelewano haupo sababu ndani ya uongozi wenyewe hawaelewani lakini hayo yote yanatokana na kujilimbikizia, mali nyingi za umma kuliko wenzio, kiongozi mmoja anakuwa na vyeo zaidi ya vitatu na hivyo yote anapokea mshahara wa pesa wanazobanwa wakulima wadogo na walala hoi kama sisi akina kabwela. Baada ya kufika masasi saa 12:00 jioni nilienda kulala kwa babu yangu mmoja pale masasi asubuhi nikapata gari lori hadi Nagaga Dispensary pale tulifika usiku nikalala asubuhi nikaanza safari kuelekea nyumbani Ng’uni huo ulikuwa mwaka 1988


Picha



Huo ndio msafara Nagaga kuelekea Ng’uni nilifika asubuhi muda Saa 1:15 asubuhi niliwakuta karibu watu wengi bado hawajaamuka wajomba, babu, bibi na ndugu zangu walifurahi sana waliponiona mwana wao ninakuja pale kijijini na baiskeli ya miguu mitatu watoto walinizunguka kupata mshangao wa kitu kama kile hayo siyo kwa watoto tu bali hata na wakubwa walipata na mshangao. Pale Ng’uni nilikaa kama siku 17 siku ya 18 nikaelekea huko Sindano ambako ndiyo nilifanya makazi yangu baada ya kumaliza elimu ya msingi kufika tu pale Sindano niliendelea na shughuli zangu za biashara ndogondogo ambazo zilinipa uwezo wa kuendesha maisha yangu bila kutegemea ombaomba kwa watu walionizunguka.

SURA 14: MAANDALIZI YA SAFARI YA KUELEKEA MT KUTAFUTA MAISHA

 Baada ya kukaa pale nyumbani Sindano niliporudi Dar es salaam niliamua kutafuta mchumba ambayoyeye ataweza kuyatunza na kuyaenzi maisha yangu huyo tulikubaliana kuwa kweli yeye yuko tayari kuishi na mimi hivyo nikafunga safari kuelekea Mtapika pale nilipeleka biashara ya madawa ya kulevya (BANGI) nilitoka SIndano nikaelekea hadi Nagaga, pale nilikaa kama masaa 8 saa 9:00 Alasili nikapata lori nikaomba yule dereva hakuwa na nongwa wala dharau aliichukua baiskeli ikapandishwa nyuma mimi mweneywe nikaa mbele pamoja na dereva kufika tu stand akaniteremsha mimi nikapanda baiskeli yangu stand, rest miesi hadi Nandembo Mtapika kufika tu nilipokelewa vyema, pale kijijini nilikaa miezi 2 tarehe 26/12/1988 nikaanza safari kurudi nyumbani baada ya kumaliza biashara zangu, hasa baada ya bus Mwamedi Ali Msepa alipopita pale Nandembo akielekea huko Masiku kwa kaka yake bwana Kiliani akaniambia brother yule bint ambayo ulimtaka kumchumbia kuna mtu anataka kumchumbia, yeye walikutana huko Nakachindu Lulindi, wao walienda huko kwenye








No comments:

Post a Comment