Habari
Kamati ya Bunge yakwama kukagua
hesabu Mwanza
Mwanza
Toleo la 310
7 Aug 2013
UHAMISHO uliofanywa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mkurugenzi na
baadhi ya wakuu wa idara katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza mapema mwaka huu,
umekwamisha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), kukagua
hesabu za halmashauri hiyo.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili
zinaeleza kuwa kamati hiyo ilishindwa kukagua hesabu za halmashauri hiyo kwa
kuwa watendaji wengi ambao wangetakiwa kujibu hoja mbalimbali za kamati hiyo ni
wageni na hivyo kwa mazingira hayo, hakuna tija ya kufanya ukaguzi huo.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Suleiman Zedi, ameliambia Raia Mwema kuwa kamati yake imeshindwa
kutimiza wajibu wake kwa kuwa si rahisi kuhoji watendaji ambao ni wageni katika
halmashauri hiyo.
"Mahesabu (hesabu) tunayokagua
yanaishia Juni mwaka huu, mkurugenzi aliyepo ninaambiwa ana miezi miwili, wale
wote waliongia mikataba na kulipa wakandarasi hawapo, kama kuna matatizo na
hoja za kujibu huyu hana majibu," alidai Zedi, ambaye ni Mbunge wa Jimbo
la Bukene, mkoani Tabora, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kamati hiyo imeagiza TAMISEMI
kuwarejesha watumishi wote baadaye mwezi huu ili kujibu hoja za kamati za
kamati hiyo na zile zilizoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa halmashauri hiyo.
Watumishi hao wanaotakiwa kurejea
ili kujibu hoja za kamati hiyo ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la
Mwanza ambaye kwa sasa ni Murugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe,
aliyekuwa mweka hazina ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Njombe, William Ntinika, aliyekuwa mchumi wa Jiji ambaye sasa ni
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Patrick
Kulangwa na aliyekuwa mhandisi wa halmashauri hiyo ambaye sasa ni Mkurugenzi
Halmashauri ya Kigoma Ujiji, Boniface Nyambele.
Pamoja na uhamisho huo kikwazo
kingine kilichofanya kamati hiyo kushindwa kukagua hesabu za halmashauri hiyo
ni pamoja na kucheleweshwa kwa vitabu vya hesabu (kufika) ofisini kwa CAG kama
inavyotakiwa na waraka wa TAMISEMI namba 2/CA.26/215.
Waraka huo unataka halmashauri
nchini kuwasilisha vitabu vyao vya hesabu kwa CAG mwezi mmoja kabla ya ukaguzi
kufanyika, lakini halmashauri ya Jiji la Mwanza imewasilisha ripoti hizo siku
chache zilizopita na kuifanya kamati hiyo kushindwa kupata muda wa kukagua.
"Lakini pia walichelewesha
vitabu vya mahesabu (sahihi hesabu) kwa hiyo hatukupata muda wa kukagua,
tumeshindwa kukagua hesabu zao," alisema Zedi.
Taarifa kutoka ndani ya Jiji la
Mwanza zinaeleza kuwa moja ya mambo ambayo yanaweza kuwaweka matatani watendaji
hao ni pamoja na mkataba walioingia na Mfuko Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
wa kununua viwanja katika eneo la Bugarika ambavyo walishindwa kuukabidhi mfuko
huo kwa wakati.
NSSF iliingia mkataba na Halmashauri
ya Jiji la Mwanza kununua jumla ya viwanja 692 kwa ajili ya kuwekeza katika
ujenzi wa nyumba za kuuza kwa wanachama wao na wananchi kwa ujumla. Katika
mkataba huo uliotiwa saini Agosti 18, 2008 kati ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Wilson Kabwe na Mkurugenzi wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau ulieleza kuwa viwanja
hivyo vitalipiwa jumla ya shilingi bilioni 1.8 ( 1,887,081,700 ) kwenye
maeneo ya Bugarika na Kiseke.
Hadi Januari, mwaka huu wakati
Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilipofanya ziara katika Halmashauri ya Jiji
la Mwanza, mgogoro huo ulikuwa ukifukuta, pamoja na NSSF kuwa ilikwisha kulipa
asilimia 80 ya fedha yote inayotakiwa kulipwa bado mfuko huo ulikuwa
haujakabidhiwa viwanja 267 vilivyoko Bugarika ambavyo thamani yake halisi ni
shilingi milioni 812.
Mkurugenzi wa uwekezaji wa
NSSF, Yacoub Kidula alisema wakati huo kuwa kama fedha hizo (Sh milioni 812)
zingewekezwa mahali pengine au katika dhamana za serikali kwa muda huo, NSSF
ingepata faida kati ya asilimia 12- 13 ambayo ni sawa na shilingi milioni 105.
Kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na
Makamu Mwenyekiti wake (kwa wakati huo) Juma Nkamia, iliagiza Mkurugenzi wa
Jiji akutane na kamati hiyo mbele ya Waziri wa TAMISEMI katika kikao cha Bunge
cha Februari, mwaka huu, ili kueleza kwa nini hawajatoa viwanja kwa NSSF,
baada ya mfuko huo kukataa kupewa viwanja mbadala katika eneo la Kishiri
lililopo Igoma nje kidogo ya Jiji, lililopendekzwa na halmashauri kuwa
halilingani thamani na eneo walilochagua awali (Bugarika) ambalo liko jirani na
Hospitali ya Rufaa ya Bugando na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Bugabdo
(CUHAS)
Hoja nyingine ambazo ziliibuliwa na
ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ni pamoja na kutotekeleza
mapendekezo ya ukaguzi ya miaka iliyopita ambayo yalifikia shilingi billioni
1.7 na kutozingatia viwango vya kimataifa vya uaandaaji wa taarifa za fedha kwa
sekta ya umma (IPSAS).
Kwa mujibu wa IPSAS, mali
zinazooneshwa kwenye taarifa ya hesabu zinazotolewa zithaminiwe na kutambuliwa
na kwamba zitaendelea kutambuliwa katika hesabu kwa kiasi ambacho
kimethaminishwa. Thamani inayotambuliwa itazingatia kutolewa kwa thamani ya
uchakavu na hasara inayotokana na ujumla wa kuharibika kwa mali.
Kinyume na mwongozo huu, uongozi wa
halmshauri ya jiji umeingia katika kundi la halmashauri 13 ambazo
hazikuthaminisha mali zake ingawa baadhi ya mali hizo zilioneshwa katika hesabu
kama ni mali ambazo hazina thamani kabisa wakati katika hali halisi mali hizo
ziliendelea kutumiwa na halmashauri.
Kutokana na hali hii, thamani ya mali
za kudumu zilizooneshwa katika taarifa za fedha za halmashauri hazitoi taswira
halisi ya halmashauri. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya CAG Jiji la Mwanza lilikuwa
na vifaa 37 ambavyo havijathaminishwa.
Hoja nyingine zilizoibuliwa na
ripoti ya CAG ya mwaka 2011/2012 ni pamoja na matumizi ya vifungu visivyohusika
yaliyofikia shilingi milioni 22.5 na watumishi 100 waliokopa zaidi ya kiwango
kinachotakiwa.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,
Halifa Hida, alipotafutwa kueleza kwa nini walichelewesha taarifa za hesabu zao
kwa CAG kinyume na waraka unavyotaka, alijibu yuko safarini na kushauri
atafutwe kaimu wake ambaye ndiye aliyekutana na kamati hiyo.
Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi huyo
Francis Mkabenga alipotafutwa na mwandishi wetu alijibu ya kuwa ana mambo mengi
ya muhimu ya kufanya kuliko hilo.
"Sisi tumewaeleza kamati
wameelewa na ndiyo maana wametupa wiki mbili, sasa hivi ninafanya mambo ya
maana zaidi kuliko hilo siwezi kuwa naeleza kila mtu, nilieleza kwenye kamati
waulize wao (kamati)," alijibu Kaimu Mkurugenzi huyo.
Soma
zaidi kuhusu:
Tufuatilie
mtandaoni:
Endelea
Kuhabarika
Toa
maoni yako
Your name
E-mail
The content of this field is kept
private and will not be shown publicly.
Homepage
Comment *
Text format
- Web page addresses and e-mail addresses turn into links automatically.
- Allowed HTML tags: <a> <em> <strong> <cite> <blockquote> <code> <ul> <ol> <li> <dl> <dt> <dd>
- Lines and paragraphs break automatically.
What code is in the image? *
Enter the characters shown in the
image.
Search
form
Search
Maoni
ya Wasomaji
· brother,suala la madawa ya kulevya hapa tanzania halina
mwenyewe,je unajua kuwa dogo r naye alinaswa na mdude kule china?kak jk akawa
mpole ,na bosi wa china akatua kuchukua tenda mbalimbali za mak
11
hours 37 min
Yametolewa
maoni mengine 2
Makala
Pendwa
Mwandishi Wetu
32,102
Waandishi Wetu
29,782
Mwandishi Wetu
27,449
Waandishi Wetu
23,736
Mwandishi Wetu
22,532
Kura
ya Maoni
Kwa wale wenye vitambulisho vya
kupiga kura, je uchaguzi wa 2010 ulipiga kura?
Ndiyo
60%
Hapana
40%
Total votes: 948
Tunapatikana
Facebook
Lango
la Wenyeji
Jina *
Siri *
· Jisajili
Wasome
zaidi Waandishi wa Raia Mwema
Copyright © 2013 Raia Mwema Newspaper Company unless otherwise
noted. All rights reserved.
Akaunti ya kigogo TANESCO yazuiwa
Toleo la 250
18 Jul 2012
- Yakutwa na zaidi ya Sh. bilioni moja, uchunguzi waendelea
- Mpango wa kupandikiza mgawo ‘feki’ wa umeme wafichuliwa
SIKU
chache baada ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Umeme (TANESCO), William Mhando na wenzake: Robert Shemhilu, Lusekelo
Kassanga na Haruna Mattambo, akaunti ya mmoja wa vigogo wa shirika hilo
ngazi ya menejimenti iliyoko katika moja ya benki nchini imezuiwa na
vyombo vya dola nchini, Raia Mwema, limeelezwa.
Akaunti ya kigogo huyo (jina la benki na la mwenye akaunti yanahifadhiwa ili kutoharibu uchunguzi unaoendelea) imekutwa na fedha zaidi ya shilingi bilioni moja na sasa inadaiwa kuzuiwa kwa baraka za mamlaka za juu.
Vyanzo kadhaa vya habari vimeeleza ya kuwa kigogo huyo amekutwa na mabilioni hayo ya fedha huku chanzo cha mapato hayo yasiyolingana na kipato chake kama mtumishi wa umma kikiwa ni utata.
Hata hivyo, wakati uchunguzi huo wa awali unaofanywa na vyombo vya dola nchini ukiwa unaendelea, kwa upande mwingine kumebainika kuwapo na kampeni kali za kuuokoa uongozi wa TANESCO unaochunguzwa kwa sasa, juhudi ambazo zimekuwa zikihusisha hata Kamati za Bunge.
Kamati za Bunge ambazo baadhi ya wajumbe wake wanahusishwa katika ‘kuokoa’ jahazi la uongozi wa TANESCO uliosimamishwa ni pamoja na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo sasa wanatajwa kuanza kumwandama Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi pamoja na Waziri Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, George Simbachawene, wanaotajwa kuwa na msimamo mkali dhidi ya kile kinachodaiwa kuwa ni uzembe na ubadhirifu ndani ya TANESCO.
Mgawo feki wa umeme
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, kwa muda mrefu sasa kumekuwa na njama za kuandaa na kufanikisha mgawo ‘feki’ wa umeme nchini kwa njia mbalimbali. Lengo la mgawo huo ni kuwanufaisha baadhi ya vigogo TANESCO kwa njia ya ununuzi wa mafuta ya kuendeshea mitambo.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na vyanzo mbalimbali vya habari ndani ya Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO, umebaini kuwa baadhi ya mitambo ya kuzalisha umeme jijini Dar es Salaam, na hasa baadhi ya mitambo iliyopo eneo la Ubungo na Tegeta imekuwa ikizimwa ili kuhalalisha migao na mpango wa ununuzi mafuta unaowaingizia fedha vigogo. Orodha ya mitambo inayozalisha umeme kwa mafuta jijini Dar es Salaam ni pamoja na IPTL, Symbion na Aggreko.
Taarifa zilizopo zinazidi kubainisha kuwa, baada ya kuzima mitambo hiyo na kusababisha mgawo wa umeme (usio wa lazima-feki), wito wa kuzalisha umeme wa mafuta hujitokeza.
Ni katika wito huo ambao msingi wake ni kupandikiza mgawo feki wa umeme, wakati mwingine Serikali hutoa fedha za ununuzi wa mafuta lakini wakati mwingine fedha hizo huchotwa kutoka TANESCO, shirika ambalo kila mwezi hukusanya shilingi karibu ya bilioni 100 kutoka kwa wateja wake.
Katika ununuzi huo wa mafuta kwa ajili ya kuendesha mitambo ili kuongeza uzalishaji wa umeme, mambo kadhaa huzingatiwa ili kunufaisha wahusika.
Jambo la kwanza ni kupatikana kwa kile kinachoitwa “ten percent” kinachogawanywa kwa waliofanikisha mpango huo. Pili, ni kuendelea kufanya wizi katika kiwango cha mafuta kilichokwishakununuliwa kwa ajili ya kuwasha mitambo husika.
Mchezo huo mchafu unadaiwa kuripotiwa kwa baadhi ya viongozi wa TANESCO lakini hapakuwa na hatua zilizopata kuchukuliwa hadi pale suala hilo lilipofika katika uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini.
“Suala hili limekuwa likifanyika kwa muda mrefu sasa, umeme unakatwa na kuzalishwa kwa kiwango cha chini ili kuibua mahitaji ya kuzalisha umeme kwa njia ya mafuta ili TANESCO wanunue. Katika ununuzi huo kuna suala la 10% na wizi wa hayo hayo mafuta yanayonunuliwa lakini pia ni manufaa kwa kampuni za uzalishaji umeme huo kwa kuwa zinakuwa zikifanya biashara kwa kuuza umeme huo TANESCO.
“Ni suala lililowahi kuripotiwa lakini likapuuzwa na menejimenti, ila miezi takriban mitatu kupita baada ya kuripotiwa kuliwahi kufanyika kikao cha wafanyakazi wote kupitia TUICO, baada ya wafanyakazi kutia shinikizo kuhusu hujuma hizi Mkurugenzi wa TANESCO, Mhando naye ndipo akadai kupata taarifa hizo hapo kwa mara ya kwanza na aliahidi kuchukua hatua,” kilieleza chanzo kimoja cha habari.
Hujuma kwa mtambo wa Kinyerezi
Hujuma nyingine inayotajwa kufanyika ndani ya TANESCO ni kuahirishwa mara kwa mara kwa mchakato wa kuanzisha mtambo wa kuzalisha umeme eneo la Kinyerezi, jijini Dar es Salaam.
Mtambo huo ambao utazalisha umeme kwa kutumia gesi, unatajwa kuwa tishio dhidi ya mtandao wa wauzaji mafuta kwa TANESCO kwa ajili ya uzalishaji umeme kwa kutumia mafuta.
“Kutokana na tishio la mradi huu utakapokamilika kuwanyima ulaji, walikuwa wakiukwamisha. Ni mradi wa megawati 240. Huu (mradi wa Kinyerezi) utaua kabisa mpango wao wa ulaji kwa kuandaa mgawo feki na kuzalisha umeme kwa mafuta. Waziri Muhongo alipoingia alihakikisha mradi unasainiwa ili kuanza....lazima wampige vita na aliwaeleza katika moja ya vikao (waziri) kuchukizwa na tabia hiyo,”
Wabunge nao watajwa
Mbunge mmoja wa Viti Maalumu kutoka mikoani (kwa sasa hatutamtaja kwa kuwa hatukufanikiwa kumpata) anadaiwa kunufaika na uongozi wa TANESCO uliosimamishwa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia,mbunge huyo anadaiwa kupewa zabuni ya kusambaza matairi kwa ajili ya magari ya TANESCO kupitia kampuni yake. Madai yanayoelekezwa kwa mbunge huyo ni kwamba, kampuni yake ilipewa zabuni baada ya zabuni hiyo ‘kuporwa’ kutoka kwa kampuni nyingine.
Lakini wakati mbunge huyo wa Viti Maalumu akihusishwa na madai hayo, mbunge mwingine na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, naye anadaiwa kuwa na maslahi na uongozi uliosimamishwa wa TANESCO.
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa katika mazungumzo yanayotajwa kwenda vizuri ili auziwe mtambo wa kufua umeme unaoitwa Kikuletwa, ulioko katika Jimbo la Hai, ili baada ya kununua aweze tena baadaye kuiuzia umeme TANESCO kama inavyofanyika kwa kampuni nyingine za uwekezaji nchini ambazo kwa muda sasa zimekuwa zikitajwa kuuza umeme kwa bei kubwa.
Raia Mwema halikufanikiwa kumpata Mbowe kusikia maelezo yake, lakini mmoja wa viongozi wa kurugezi za chama hicho, John Mrema, amemweleza mwandishi wetu kuwa anayetaka kununua mtambo huo si Mbowe binafsi bali ni Halmashauri ya Wilaya ya Hai.
“Mbowe kama mbunge alikuwa akisaidia kufanikisha hilo. Mpango uliopo ni kununua mtambo huo wa siku nyingi ambao hautumiki ni kuukarabati na kisha kuanza kuzalisha umeme ambao sehemu itatumiwa na wananchi wa Hai na kiasi kingine cha umeme kitauzwa TANESCO,” alisema Mrema.
Suala la kusimamishwa kwa uongozi huo wa juu wa TANESCO limevuta hisia nyingi huku makundi ya watu wakipita huku na kule kujaribu kubatilisha uamuzi huo, mengine yakidai kwamba taratibu za kuusimamisha zimekiukwa, mengine yakivurumisha tuhuma nzito dhidi ya uongozi wa wizara na mengine yakitaka Bodi nzima ya TANESCO iondolewe kwa vile baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo wamekuwa wakifanya biashara ya mafuta na shirika hilo.
Raia Mwema limefahamishwa kwamba timu ya uongozi wa wizara jana ilikuwa Dodoma ambako iliitwa kwenda kujieleza mbele ya Kamati za Bunge zinazohusiana na TANESCO.
Tarifa zaidi zilizopatikana tukienda mitamboni zilieleza kwamba pamoja na kukutana na kamati hizo, timu hiyo ya wizara imeomba kukutana kwanza na kamati ya CCM ambako mtoa habari wetu ametufahamisha kwamba patamwagwa kila kitu hadharani kuhusiana na nani wanahujumu TANESCO, nani wanaofadika nayo na kwa njia zipi.
Kusimamishwa kwa Injinia Mhando na wenzake kulikuja kiasi cha siku tatu tu baada ya Raia Mwema kuripoti taarifa za kuwako makundi ya wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na wenzao ndani ya mashirika na taasisi tanzu za wizara hiyo, wanaohujumu jitihada za sasa za kuisuka upya wizara na taasisi na mashirika yake.
Jitihada hizo, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari serikalini, zimekuwa pia zikiwahusisha kwa karibu baadhi ya wenyeviti wa bodi za mashirika na taasisi hizo na watendaji wakuu wake ambao wanahisi ya kuwa, kwa mazingira mapya wizarani, ajira zao zinakaribia ukingoni kutokana na ama utendaji binafsi usiokidhi au kwa kushindwa kudhibiti uozo katika taasisi na mashirika yao.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mtandao wa makundi hayo ulioungana ulikuwa ukiendesha kampeni ya kuukataa uongozi wa wizara kwa madai kwamba umekuwa ukiendesha mambo kibabe.
Raia Mwema limedokezwa pia kwamba nje ya wizara, taasisi na mashirika yake, mtandao huo unaungwa mkono na baadhi ya wabunge, wengine wakiwa katika kamati zinazohusiana na wizara hiyo, na kwamba mipango iliyokuwa inasukwa ili kupeleka ujumbe kwa mamlaka husika kuwa uongozi wa wizara haufai, uondolewe, ni pamoja na kukwamisha bajeti ya wizara itakayowasilishwa bungeni wiki ijayo.
Hoja nyingine zanazodaiwa kushadidiwa na mtandao huo kama sababu za ziada kutaka mabadiliko ya uongozi wizarani ni kuwa Waziri mpya, Profesa Sospeter Muhongo, si mwanasiasa, ubunge wake uliompa uwaziri umetokana na yeye kuteuliwa na hilo linawakera baadhi ya wabunge wa majimbo ambao wanaona si vyema wao kuachwa, mtu wa “kuja” akapewa nafasi hiyo kubwa tena katika wizara inayotajwa kuwa tajiri na yenye ulaji kama ya Nishati na Madini.
Ukiacha hilo, Raia Mwema limeambiwa pia ya kuwa madai mengine ni suala ambalo chimbuko lake ni ukabila. Waziri Profesa Muhongo anatoka Mkoa wa Mara ambako ndiko anakotoka pia Katibu Mkuu, Eliachim Maswi, ingawa inafahamika kwamba wanatoka katika maeneo mawili tofauti ya mkoa huo. Kwa mujibu wa madai ya wana mtandao huo, Profesa Muhongo na Maswi kwa kutoka katika Mkoa mmoja na sasa wanafanya kazi ofisi moja ni tatizo.
Alipoulizwa na Raia Mwema juu ya madai hayo, mwanzoni mwa wiki iliyopita, Maswi alisema hakuwa na namna ya kuzuia watu wasizungumze wanayoyataka. Alisema yawepo au yasiwepo, yeye na timu wanayoijenga wizarani wameamua kufanya kazi ili kuleta tija katika maeneo waliyokabidhiwa kuyasimamia.
“Rais Jakaya Kikwete aliyetuteua hakufanya hivyo ili tuje hapa tuchezecheze. Tumepewa majukumu ya kutekeleza. Hebu niambie, nyumbani kwako siku hizi umeme unakatika mara ngapi?
“Ukiona kuna mawazo kama hayo, ujue tunafanya kazi. Sisi hatutajali yanayosemwa, kipimo chetu ni kama umma unaridhika. Kama unaona baadhi ya kero zilizokuwapo, zilizokuwa ndani ya uwezo wetu, sasa zimepungua kwenye vitu kama umeme, na kama tumeanza kupata stahili yetu kwenye maeneo kama ya migodi ujue wizarani sasa kuna wachapakazi,” alisema Maswi.
Katibu Mkuu Maswi aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Kaimu Katibu Mkuu katikati ya Julai mwaka jana, kiasi cha mwaka mmoja uliopita, akichukua nafasi iliyokuwa imeachwa na David Jairo aliyekuwa ametuhumiwa na Bunge, pamoja na mambo mengine, kwa ubadhirifu.
Aidha, Profesa Muhongo, mmoja wa Watanzania wachache wataalamu wa jiolojia, amejiunga serikalini mwanzoni mwa Mei, mwaka huu, baada ya kuteuliwa na Rais Kikwete kwanza kama mbunge kupitia nafasi 10 za Rais kuteua wabunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ni Shirika la Umeme (TANESCO) ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Jenerali mstaafu na mkuu wa zamani wa Majeshi, Robert Mboma, Mtendaji wake Mkuu ni Mhandisi Godfrey Mhando.
Mengine ni EWURA ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Simon Sayore; huku Mtendaji Mkuu akiwa Haruna Masebu; Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Balozi Ami Mpungwe na Mtendaji Mkuu ni Dk. Dk Lutengano Mwakahesya; Wakala wa Madini (TMAA) ambalo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Dk. Yamungu Kayandabila, Mtendaji Mkuu akiwa Mhandisi Paul Masanja.
Mengine ni STAMICO ambalo Mwenyekiti wa Bodi ni Ramadhani Omari Hatibu, Mtendaji Mkuu akiwa Grey Mwakalukwa; GST lililo chini ya Uenyekiti wa Bodi wa Profesa Idrissa Kikula na Mendaji Mkuu akiwa Profesa Abdul Mruma na TPDC ambalo Mwenyekiti wake ni Michael Mwanda na Mtendaji Mkuu ni Yona Kilagane.

Tufuatilie mtandaoni:
Endelea Kuhabarika
Maoni ya Wasomaji
huyo kigogo waliyemfungia
huyo
kigogo waliyemfungia akaunti yake wanamuonea tu. mbona yule waziri
anayesubiri kuota ndoto anajenga hoteli ya mabilioni kule mtwara? mbona
yeye hanyanganywi?? halafu kuna waziri kijana ndani ya miaka 3
alijipatia magorofa na majumba ya bei mbaya. kwanini yeye ilionekana ni
kitu cha kawaida??
Ndg. Kinyonga.
Ndg. Kinyonga.
tatizo linapotokea kinachohitajika ni hatua za kulishughulikia. huwezi kusema uliache kama lilivyo eti kwasababu kuna matatizo mengine kama hayo sehemu nyingine. vinginevyo hiyo "wamemuonea" maana yake nini?. aachwe eti kwasababu kuna wengine?. ulipaswa kushauri na hao wengine washughulikiwe hivyohivyo na sio kutangaza "wamemuonea" mtu ambaye anatuhumiwa kuihujumu nchi. hiyo ina maana unaunga mkono vitendo vya kifisadi. acha ndg. yangu namna hiyo sio uungwana.!

sisi watanzania watu wa ajabu
sisi
watanzania watu wa ajabu sana, kila kukicha tunalalamika ili au lile
tunapopata watu wa kutuletea majawabu ya matatizo yetu pia tunalalamika
ni kipi hasa tunataka jamani?!
Hatuwezi kuwakamata mafisadi
Hatuwezi
kuwakamata mafisadi wote siku moja, huu ni mwanzo na ni hatua nzuri
watu wa Mara hawajui blaa blaa walipo ni wachapakazi tuu. Angalia usije
ukawa ndugu wa kigogo huyo aliyefungiwa akaunti.
Nyoka ni mtoto wa nyoka;
Nyoka ni mtoto wa nyoka; ukimuua, yule aliyemzaa ataza mwingine. Dawa ni kuua yule nyoka anayewazaa nyoka hao wengine.
Ubinafsi haujali umri,cheo
Ubinafsi
haujali umri,cheo,elimu,mamlaka..,haujali hasara,maisha ya
wengine,..Watanzania ni wakati wa kubadilika.Kila mtu anahitaji maisha
bora.Tuwe mawakili wazuri wa mali za umma kwa manufaa ya umma.Utajiri
upatikanao kwa hila hautuongezei maisha marefu,bali AIBU ya sasa na ya
Baadaye.Mungu Ibariki Tanzania.Mungu wabariki Viongozi wetu, watangulize
TAIFA kwanza,Utumishi kwanza.
Kwa kweli TANESCO wametuchosa
Kwa
kweli TANESCO wametuchosa Watanzania! Limekuwa shirika sugu na chafu
kwa muda mrefu. Swala kubwa kwa TANESCO ni wafanyakazi duni wasiojua
wajibu wao na kuendekeza rushwa. Mfano mzuri ni viituo vile vilivyoweka
kama vile cha TAZARA, Kinyerezi, n.k. Mambo yanayofanyika kwenye vituo
hivyo ni uozo mtupu! ambao uongozi wa juu usipofuatilia shirika
litaendelea kuangamia huku wachache wakijinufaisha na jasho la umma.
Watanzania sasa tumechoka
Watanzania
sasa tumechoka kusikia wanasiasa wanayumbisha nchi mpaka inafikia
Bunge au Wabunge kutaka kuhalalisha Ufisadi, kweli inauma sana .
Tunawasubiri na kamati zao waje sie wananchi sio wajinga tunaona na
kusikia .
Mtu mwema na muadilifu anapigwa vita eti kwa maslahi ya wachache sasa tunasubiri hiyo kamati ije.
Tutapita nchi nzima kuwatangaza wote hao kwa majina bila kujali chama , maana nawapinzani nao wamo katika ufisadi huo wanachi wawaadhibu maana tulidhani wapinzani ni waadilifu kumbe mafisadi watupu.
Tuwaunge mkono viongozi wanaotetea wananchi

Kama kweli tunataka kuwajuwa
Kama
kweli tunataka kuwajuwa Viongozi wetu basi tukubali kama wote ni
wezi,majangili,majambazi,waasherati na wahuni kupindukia.hizi ndio sifa
zao na wako madarakani kwa kuogopana na kufichiana siri zao.
Kila mmoja ana scandal kumshinda mwenzake ,nani atamkamata mwenziwe ?. Watanzania wacheni kupepea mwiku ushapowa huo kuleeenni tuuuuuuuuuuu

Toa maoni yako
Copyright © 2013 Raia Mwema Newspaper Company unless otherwise noted. All rights reserved.
ShareThis Copy and Paste
No comments:
Post a Comment