Habari
Kamati ya Bunge yakwama kukagua
hesabu Mwanza
Mwanza
Toleo la 310
7 Aug 2013
UHAMISHO uliofanywa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mkurugenzi na
baadhi ya wakuu wa idara katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza mapema mwaka huu,
umekwamisha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), kukagua
hesabu za halmashauri hiyo.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili
zinaeleza kuwa kamati hiyo ilishindwa kukagua hesabu za halmashauri hiyo kwa
kuwa watendaji wengi ambao wangetakiwa kujibu hoja mbalimbali za kamati hiyo ni
wageni na hivyo kwa mazingira hayo, hakuna tija ya kufanya ukaguzi huo.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Suleiman Zedi, ameliambia Raia Mwema kuwa kamati yake imeshindwa
kutimiza wajibu wake kwa kuwa si rahisi kuhoji watendaji ambao ni wageni katika
halmashauri hiyo.
"Mahesabu (hesabu) tunayokagua
yanaishia Juni mwaka huu, mkurugenzi aliyepo ninaambiwa ana miezi miwili, wale
wote waliongia mikataba na kulipa wakandarasi hawapo, kama kuna matatizo na
hoja za kujibu huyu hana majibu," alidai Zedi, ambaye ni Mbunge wa Jimbo
la Bukene, mkoani Tabora, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kamati hiyo imeagiza TAMISEMI
kuwarejesha watumishi wote baadaye mwezi huu ili kujibu hoja za kamati za
kamati hiyo na zile zilizoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa halmashauri hiyo.
Watumishi hao wanaotakiwa kurejea
ili kujibu hoja za kamati hiyo ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la
Mwanza ambaye kwa sasa ni Murugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe,
aliyekuwa mweka hazina ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Njombe, William Ntinika, aliyekuwa mchumi wa Jiji ambaye sasa ni
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga Patrick
Kulangwa na aliyekuwa mhandisi wa halmashauri hiyo ambaye sasa ni Mkurugenzi
Halmashauri ya Kigoma Ujiji, Boniface Nyambele.
Pamoja na uhamisho huo kikwazo
kingine kilichofanya kamati hiyo kushindwa kukagua hesabu za halmashauri hiyo
ni pamoja na kucheleweshwa kwa vitabu vya hesabu (kufika) ofisini kwa CAG kama
inavyotakiwa na waraka wa TAMISEMI namba 2/CA.26/215.
Waraka huo unataka halmashauri
nchini kuwasilisha vitabu vyao vya hesabu kwa CAG mwezi mmoja kabla ya ukaguzi
kufanyika, lakini halmashauri ya Jiji la Mwanza imewasilisha ripoti hizo siku
chache zilizopita na kuifanya kamati hiyo kushindwa kupata muda wa kukagua.
"Lakini pia walichelewesha
vitabu vya mahesabu (sahihi hesabu) kwa hiyo hatukupata muda wa kukagua,
tumeshindwa kukagua hesabu zao," alisema Zedi.
Taarifa kutoka ndani ya Jiji la
Mwanza zinaeleza kuwa moja ya mambo ambayo yanaweza kuwaweka matatani watendaji
hao ni pamoja na mkataba walioingia na Mfuko Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
wa kununua viwanja katika eneo la Bugarika ambavyo walishindwa kuukabidhi mfuko
huo kwa wakati.
NSSF iliingia mkataba na Halmashauri
ya Jiji la Mwanza kununua jumla ya viwanja 692 kwa ajili ya kuwekeza katika
ujenzi wa nyumba za kuuza kwa wanachama wao na wananchi kwa ujumla. Katika
mkataba huo uliotiwa saini Agosti 18, 2008 kati ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Wilson Kabwe na Mkurugenzi wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau ulieleza kuwa viwanja
hivyo vitalipiwa jumla ya shilingi bilioni 1.8 ( 1,887,081,700 ) kwenye
maeneo ya Bugarika na Kiseke.
Hadi Januari, mwaka huu wakati
Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilipofanya ziara katika Halmashauri ya Jiji
la Mwanza, mgogoro huo ulikuwa ukifukuta, pamoja na NSSF kuwa ilikwisha kulipa
asilimia 80 ya fedha yote inayotakiwa kulipwa bado mfuko huo ulikuwa
haujakabidhiwa viwanja 267 vilivyoko Bugarika ambavyo thamani yake halisi ni
shilingi milioni 812.
Mkurugenzi wa uwekezaji wa
NSSF, Yacoub Kidula alisema wakati huo kuwa kama fedha hizo (Sh milioni 812)
zingewekezwa mahali pengine au katika dhamana za serikali kwa muda huo, NSSF
ingepata faida kati ya asilimia 12- 13 ambayo ni sawa na shilingi milioni 105.
Kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na
Makamu Mwenyekiti wake (kwa wakati huo) Juma Nkamia, iliagiza Mkurugenzi wa
Jiji akutane na kamati hiyo mbele ya Waziri wa TAMISEMI katika kikao cha Bunge
cha Februari, mwaka huu, ili kueleza kwa nini hawajatoa viwanja kwa NSSF,
baada ya mfuko huo kukataa kupewa viwanja mbadala katika eneo la Kishiri
lililopo Igoma nje kidogo ya Jiji, lililopendekzwa na halmashauri kuwa
halilingani thamani na eneo walilochagua awali (Bugarika) ambalo liko jirani na
Hospitali ya Rufaa ya Bugando na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Bugabdo
(CUHAS)
Hoja nyingine ambazo ziliibuliwa na
ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ni pamoja na kutotekeleza
mapendekezo ya ukaguzi ya miaka iliyopita ambayo yalifikia shilingi billioni
1.7 na kutozingatia viwango vya kimataifa vya uaandaaji wa taarifa za fedha kwa
sekta ya umma (IPSAS).
Kwa mujibu wa IPSAS, mali
zinazooneshwa kwenye taarifa ya hesabu zinazotolewa zithaminiwe na kutambuliwa
na kwamba zitaendelea kutambuliwa katika hesabu kwa kiasi ambacho
kimethaminishwa. Thamani inayotambuliwa itazingatia kutolewa kwa thamani ya
uchakavu na hasara inayotokana na ujumla wa kuharibika kwa mali.
Kinyume na mwongozo huu, uongozi wa
halmshauri ya jiji umeingia katika kundi la halmashauri 13 ambazo
hazikuthaminisha mali zake ingawa baadhi ya mali hizo zilioneshwa katika hesabu
kama ni mali ambazo hazina thamani kabisa wakati katika hali halisi mali hizo
ziliendelea kutumiwa na halmashauri.
Kutokana na hali hii, thamani ya mali
za kudumu zilizooneshwa katika taarifa za fedha za halmashauri hazitoi taswira
halisi ya halmashauri. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya CAG Jiji la Mwanza lilikuwa
na vifaa 37 ambavyo havijathaminishwa.
Hoja nyingine zilizoibuliwa na
ripoti ya CAG ya mwaka 2011/2012 ni pamoja na matumizi ya vifungu visivyohusika
yaliyofikia shilingi milioni 22.5 na watumishi 100 waliokopa zaidi ya kiwango
kinachotakiwa.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,
Halifa Hida, alipotafutwa kueleza kwa nini walichelewesha taarifa za hesabu zao
kwa CAG kinyume na waraka unavyotaka, alijibu yuko safarini na kushauri
atafutwe kaimu wake ambaye ndiye aliyekutana na kamati hiyo.
Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi huyo
Francis Mkabenga alipotafutwa na mwandishi wetu alijibu ya kuwa ana mambo mengi
ya muhimu ya kufanya kuliko hilo.
"Sisi tumewaeleza kamati
wameelewa na ndiyo maana wametupa wiki mbili, sasa hivi ninafanya mambo ya
maana zaidi kuliko hilo siwezi kuwa naeleza kila mtu, nilieleza kwenye kamati
waulize wao (kamati)," alijibu Kaimu Mkurugenzi huyo.
Soma
zaidi kuhusu:
Tufuatilie
mtandaoni:
Endelea
Kuhabarika
Toa
maoni yako
Your name
E-mail
The content of this field is kept
private and will not be shown publicly.
Homepage
Comment *
Text format
- Web page addresses and e-mail addresses turn into links automatically.
- Allowed HTML tags: <a> <em> <strong> <cite> <blockquote> <code> <ul> <ol> <li> <dl> <dt> <dd>
- Lines and paragraphs break automatically.
What code is in the image? *
Enter the characters shown in the
image.
Search
form
Search
Maoni
ya Wasomaji
· brother,suala la madawa ya kulevya hapa tanzania halina
mwenyewe,je unajua kuwa dogo r naye alinaswa na mdude kule china?kak jk akawa
mpole ,na bosi wa china akatua kuchukua tenda mbalimbali za mak
11
hours 37 min
Yametolewa
maoni mengine 2
Makala
Pendwa
Mwandishi Wetu
32,102
Waandishi Wetu
29,782
Mwandishi Wetu
27,449
Waandishi Wetu
23,736
Mwandishi Wetu
22,532
Kura
ya Maoni
Kwa wale wenye vitambulisho vya
kupiga kura, je uchaguzi wa 2010 ulipiga kura?
Ndiyo
60%
Hapana
40%
Total votes: 948
Tunapatikana
Facebook
Lango
la Wenyeji
Jina *
Siri *
· Jisajili
Wasome
zaidi Waandishi wa Raia Mwema
Copyright © 2013 Raia Mwema Newspaper Company unless otherwise
noted. All rights reserved.
No comments:
Post a Comment